Jumatano 24 Desemba 2025 - 21:00
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Iraq akutana na Ayatullah Al-Udhma Sheikh Bashir Hussein Najafi

Hawza/ Clemens Simetner, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Iraq, akiwa ameambatana na ujumbe wake, alikutana na Ayatullah Al-Udhma Sheikh Bashir Hussein Najafi katika mji mtukufu wa Najaf Ashraf.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika mkutano huo walijadiliana kuhusiana na mkusanyiko wa masuala ya kibinadamu katika ngazi ya kimataifa, pamoja na maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda. Ayatullah Al-Udhma Sheikh Bashir Hussein Najafi, katika maelezo yake, alisisitiza juu ya majukumu rasmi ya misheni za kidiplomasia, akabainisha kuwa; uwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Iraq unapaswa kutekeleza wajibu wake kwa namna itakayokuwa kwenye kuyahudumia mataifa na kwa dhati na kuchunga maslahi ya umma.

Vilevile, alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Ulaya katika kutekeleza jukumu lenye athari chanya kwenye kuboresha hali ya Iraq katika nyanja mbalimbali, zikiwemo uchumi, elimu na masuala ya kijamii, na akaongeza kuwa; ushirikiano wa kimataifa utakuwa na manufaa pale tu utakapoambatana na uelewa wa kina wa mahitaji halisi ya jamii pamoja na kuheshimu maadili na uwezo wa ndani wa nchi husika.

Ayatullah Bashir Najafi, akirejelea umuhimu wa kuheshimu utambulisho wa mataifa na urithi wao wa ustaarabu, alisisitiza kwa kusema: watu wa Iraq ni warithi wa ustaarabu wa kale na wenye mizizi imara, ambao historia yake inarejea katika nyakati za mwanzo kabisa za kuundwa kwa ustaarabu wa mwanadamu; kwa hiyo, taasisi na mashirika ya kimataifa yanapaswa, katika mahusiano yao na Iraq, kuzingatia ukweli huu wa kihistoria na kitamaduni.

Katika kuendeleza mkutano huo, Clemens Simetner, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Iraq, aliwasilisha taarifa kuhusu shughuli na majukumu ya misheni ya kidiplomasia ya Umoja wa Ulaya nchini humo, na akasema: Umoja wa Ulaya unapendelea kuthibitisha maendeleo na kuinua kiwango cha ustawi wa jumla kwa wananchi wa Iraq na unaona kuwa ni miongoni mwa vipaumbele vyake, na katika mwelekeo huo, unaupa umuhimu mkubwa ushirikiano na mazungumzo na taasisi za kidini na kijamii.

Aidha, alimshukuru Ayatullah al-Udhma Sheikh Bashir Hussein Najafi kwa mapokezi mazuri na kwa kutenga muda wake kwa ajili ya mkutano huo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha